Monday, June 8, 2015

SIWEMA wa NAY wa Mitego Yamemshuka..Ajirudi na Kumpigia Goti Nay wa Mitego ili Warudiane Kumlea Mtoto Pamoja..Nay Asema Haya


PAMOJA NA MAJIGAMBO LUKUKI KUTOKA KWA SIWEMA HATIMAYE KETE IMEGEUKA NA KUJIKUTA AKIMWANGUKIA NAY WA MITEGO ILI WARUDIA TAYARI KWA KULEA PAMOJA MTOTO WAO!! Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni ndugu wa Siwema kilieleza kuwa, pamoja na  maneno ya shombo aliyommwagia Nay wakati wanaachana, mrembo huyo kwa sasa ameweka nyodo kando na kuomba asamehewe..... Kilidai kwamba hivi karibuni, mmoja wa dada wa Siwema (jina linahifadhiwa) amekuwa akimpigia simu Nay akimuomba arudishe moyo wake kwa Siwema, kwani tangu aachane naye mambo yamekuwa yakienda kombo ikiwemo ule msala wa kesi inayoendelea mahakamani ya kujipatia mali isivyo kihalali.

Baada ya kumwagiwa ubuyu huo,  lilituma kijumbe kumfikishia Nay ombi hilo la Siwema ambapo alikuwa na haya ya kusema:

  • Kweli nimepokea simu za msamaha. Nimemsamehe lakini siwezi kurudiana naye.

Kwa upande wake mama Nay alisema yeye ndiye alikuwa mtetezi wake lakini kwa sasa hataki kusikia ishu hiyo.
GPL


Unknown Web Developer

Morbi aliquam fringilla nisl. Pellentesque eleifend condimentum tellus, vel vulputate tortor malesuada sit amet. Aliquam vel vestibulum metus. Aenean ut mi aucto.

No comments:

Post a Comment