Jennifer Lopez azua kizaazaa Morocco, waziri wa mawasiliano aombwa kujiuzulu
Nyota wa muziki kutoka nchini Marekani anaefahamika kwa jina la Jennifer Lopez amezua gumzo na tatizo nchini Morocco kutokana na mavazi aliovalia katika tamasha lake nchini humo.
Waziri wa mawasiliano wa Moroco bwana Mustapha Khalfi ameombwa kujiuzulu baada ya kutoa ruhusa kuoneshwa sha tamasha la msanii huyo katika kituo cha televisheno cha taifa.
Wanachama wa chama cha JD nchini Morocco walifahamisha kuwa tamasha la msanii huyo nchini Morocco katika maonesho ya Mawazine jijini Rabat ni ukeukwaji wa mila na desturi za Morocco.
Taarifa kutoka nchini Morocco zinafahamisha kuwa waziri Khalfi ametupilia mbali ombi linalomtaka kujiuzulu.
Tamasha hilo lilihudhuriwa takriban na watu 160,000 Ijumaa na kuoneshwa katika kituo cha televisheni ya taifa cha 2M.
Baadhi ya wabunge wameliomba baraza la utamaduni na mawasiliano kuandaa mkutano ili kujadili sababu zilizopelekea tamasha hilo kuonesha katika kituo cha 2M.
No comments:
Post a Comment